Posts

Showing posts from March, 2017

Mbowe Azua Jipya..Adai Bajeti ya Serikali Haitekeleziki..Wajiandaa Kuipinga Bungeni

Image
                                       Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wataipinga bungeni bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwani haina msaada wowote kwa wananchi wa hali ya chini na wanaamini fedha hizo hazitapatikana kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbowe amesisitiza mwaka jana wabunge wa kambi ya upinzani walieleza wazi kuwa bajeti ya mwaka huu isingetekelezeka na ndio kilichotokea kwani mpaka sasa asilimia 34 pekee ya pesa zote za maendeleo ndizo zimetolewa.

Tathimini ya uharibifu wa kimbunga Debbie yaanza kufanyika Australia

Image
Maofisa katika jimbo la Queensland nchini Australia wameanza kufanya tathimin ya madhara makubwa yaliyosababishwa na kimbuka Debbie, huku baadhi ya maeneo yakiwa hayawezi kufikiwa kutokana na barabara kuharibika na kujifunga kabisa. Baadhi raia wameuelezea mji wa Bowen kwamba umeharibika na kuwa kama ukanda wa vita kutokana na kubomoka kwa majengo na mashamba ya ndizi. Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull, amesema kuwa serikali imejiandaa vyema kukabiliana na madhara ya kimbunga hicho kilichoyakumba maeneo hayo. Hata hivyo mamlaka nchini Austarilia zimeonya kuwa eneo la Pwani ya kaskazini mashariki nchini humo lililopo kilomita 1300 linatarajiwa kukumbwa na mafuriko ikiwa ni matokeo ya kimbunga hicho

Huu Ndio Ujumbe wa Mbunge Husein Bashe wa CCM,Ambao Umekuwa Gumzo Mitandaoni

Image
                            Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe (CCM)amechapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno haya. “Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo‘ “Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu ‘Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru‘ –Hussein Bashe ‘Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu. ‘Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu ‘Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la k...

Madaktari Kenya Wawaonya Madaktari wa Tanzania Wanaotaka Kwenda Kenya

Image
  Chama cha Madaktari wa Kenya (KMPDU), kimewataka wenzao wa Tanzania wasikubali kusaini mkataba wowote wa kwenda Kenya kabla mgogoro wao na Serikali haujatatuliwa. Taarifa ya KMPDU  inasema haina tatizo na uwezo ama mafunzo ya madaktari wa Tanzania na protokali ya leseni za madaktari inayotambulika na Baraza na Bodi za nchi za Afrika Mashariki. “Lakini tunapenda kuwataarifu kwamba kwa miaka miwili iliyopita, madaktari wa Kenya wamekuwa wakihangaika na Serikali ya Kenya kuhusu idadi yetu na kukataliwa kwa kile Serikali na Wizara ya Afya ilichosema ni ukomo wa bajeti jambo ambalo lilikuwa likichochea mgomo uliokwisha wiki moja iliyopita. “Tunawashukuru kwa kutuunga mkono wakati wa mgomo wetu uliodumu kwa siku 100. “Tumeona makubaliano ya Serikali ya Kenya na Tanzania wa kuleta madaktari 500 ili kuleta uwiano (ration) kati ya wagonjwa na madaktari kwenye pengo lililopo nchini kwa sasa. “Hadi kufikia Mei 2017, kutakuwa na madaktari wanaokadiriwa kufikia 1,400 ambao ...

#BREAKING: Maamuzi ya vyombo vya habari Tanzania kuhusu RC Makonda

Image
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo March 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo. TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.     Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda     Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.     Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye. Unaweza kusoma kila kitu kwenye tamko hili hapa chini.

Ruge athibitisha Makonda kuivamia Clouds media akiwa na silaha

Image
Mkurugenzi wa Vipindi na Uendeshaji  wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amehojiwa leo katika kipindi cha 360 cha televisheni ya Clouds na kuthibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho.. Akizungumza na watangazaji wa kipindi hicho, Ruge aliongea kwa hisia na kuthibitisha kuwa tukio hilo lilitokea siku ya ijumaa ya tarehe 17 majira ya usiku kituoni hapo. Alieleza kuwa, siku ya Alhamisi RC makonda alifika katika kituo hicho na kuongea na watangazaji wa SHILAWADU, Sudy Brown na Qwisser ambapo alisema kuwa wanapiga tu stori. “Mtangazaji mmoja alinifuata akaniambia wamefanya mahojiano na mwanamke anayedaiwa kuwa amezaa na Askofu Gwajima lakini Gwajima mwenyewe hawajampata. Niliwaambia watangazaji kama hawajampata Gwajima, basi kipindi hicho kisirushwe kwa kuwa hakina ‘balance’ na wamwambie Makonda.” “Gwajima alinipigia simu akisema amesikia kuwa kuna kipindi chake, nikamwambia kuwa hakitarushwa kwa sababu hatujasikia pande zote. Na nikampi...

Alichokisema Zitto Kabwe Baada ya Kikwete Kuzindua Taasisi Yake ...!!!!

Image
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete jana amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu. Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia akaunti yake ya Facebook: “Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri

Makonda Arudi Bongo kimya Kimya,Leo Aonekana Kurasini Akizindua Barabara..!!!!

Image
                              Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amezindua barabara ya Shimo la Udongo, Kilwa EPZ iliyopo kurasini ya Kilomita moja; Iliyojengwa kwa kiwango cha zege na kampuni ya wazalendo ya Grant Tech iliyogharimu takribani milioni 350.

Kinana Amjibu Kikwete Juu ya Mabadiliko ya CCM..!!!

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ndugu Abdurhaman Kinana amesema mabadiliko wanayoyafanya ndani ya chama hicho yatakuwa yanagusa sehemu muhimu kama Katiba ndani ya CCM, kanuni za uchaguzi pamoja na kanuni za Jumuiya. Hayo aliyabaanisha katika mkutano Maalum wa mabadiliko uliofanyikia Jijini Dodoma, huku akibainisha baadhi ya vitu na kusema mageuzi hayo hayamlengi mtu wala kikundi chochote bali yanalenga kutoa ufanisi ndani ya chama hicho. “CCM imekuwa na utamaduni wa mabadilko na imeshafanya hivyo mara 15 na awamu hii ni mara ya 16 sasa dhamira ikiwa ni kuweka uhai, ubora na ushindi wa CCM”. Alisema Kinana Aidha Katibu huyo ametaja mabadiliko waliyoyakusudia kuyafanya kuwa ni kupunguza utitiri wa vyeo, idadi ya vikao viwe vichache ambavyo vitakuwa na tija kwao pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe. Kwa upande mwingine Kinana amefananisha mabadiliko hayo na vyama vingine vikongwe duniani ikiwemo chama cha Kikomunist cha China ambacho wanachama wengi lakini idadi ya wajumbe...

Bashe, Musukuma, Malima Watiwa mbaroni Kwa Kufanya Vurugu Katika Mkutano wa CCM

Image
Wabunge Hussein Bashe wa Nzega Mjini na Joseph Kasheku wa Geita wakiwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Kisarawe, Adam Malima wamehojiwa polisi na kisha kuachiwa baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za kuvuruga mkutano mkuu wa CCM Inaelezwa kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM, ambao unatarajiwa kufanyika kesho, Machi 12 mjini Dodoma walikuwa wakipanga njama za kuvuruga mkutano huo kwa kugawa pesa kwa baadhi ya wajumbe. Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao, kwa ajili ya mahojiano, lakini amesema kuwa baada ya mahojiano, wabunge hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kujidhamini wao wenyewe. "Walikuwa wanahojiwa tu lakini kwa sasa wameshaachiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba wanagawa hela wanapanga kuvuruga mkutano wa CCM, wamejidhamini wenyewe, na upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama ni kweli" Amesema Kamanda Mambosasa Kuhusu endapo watu hao walikutwa na pesa, Kamanda amesema mmoja kati yao amekutwa na pesa la...

Warioba Apigilia Msumari Baa la Njaa Nchini...

Image
                 Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Sinde Warioba amesema haina haja ya kubishana kama kuna njaa au upungufu wa chakula kwani dalili zinaonyesha tatizo hilo litatupata na haitakuwa mara ya kwanza kwani limeshawahi kutokea. Amesema kuwa wakati wa nyuma tatizo kama hilo lilipotokea watu walishirikiana kusaidia kuwapa wakulima maarifa na taarifa za hali ya hewa ili waweze kukabiliana na tatizo. Ametolea mfano njaa inavyoathiri nchi za Somalia, Kenya na Nigeria kwa sasa ambapo watu na mifugo wamefariki na kusema mabishano hayasaidii. Ameyasema hayo yote katika Kongamano la wanawake katika Uongozi linaloendelea katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mabadiliko ya CCM Kusomba Vigogo 11,Wamo Mawaziri,Wabunge na Makada Maarufu..!!!

Image
  Wakati mabadiliko ya katiba yatawaengua vigogo 11 katika uongozi wa CCM walio na kofia zaidi ya moja, hatima ya idadi kama hiyo ya wanachama wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, itajulikana kesho. CCM inatarajia kupitisha mabadiliko makubwa ya katiba, ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe katika vikao vya juu na pia kupunguza kofia za uongozi mwanachama mwenye cheo ndani ya chama, ubunge au serikalini. Mabadiliko hayo yalipendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 13 mwaka jana. Mabadiliko hayo yalitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliyemaliza muda wake, Nape Nnauye kwamba muundo wa chama umebadilika na mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa CCM, Toleo la 2012, Kifungu cha 22 na 23. Nape alizitaja nafasi hizo kuwa ni mwenyekiti wa tawi, kijiji au mtaa, kata/wadi, jimbo, wilaya na mkoa. W...

Waziri aonya wasimamizi wa misitu

Image
                              WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameonya tabia ya wasimamizi wa misitu kuingia mikataba binafsi na wamiliki wa mifugo hasa ng'ombe kulisha katika hifadhi za misitu nchini. Amesema kitendo hicho kimesababisha kuharibika kwa uoto wa asili na kuleta uharibifu mkubwa katika hifadhi za misitu. Akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu nchini (TFS) mjini Dodoma, Profesa Maghembe amesema misitu nchini ipo hatarini kutoweka kutokana na uamuzi binafsi unaofanywa na watu wenye dhamana ya kutunza misitu. Amesema wanyama wanaoingizwa ndani ya misitu wakiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo wanavuruga utaratibu wa asili na kuua vyanzo vya maji, hivyo kuleta ukame. Waziri Maghembe amesema hifadhi ya misitu mingi kwa sasa imekuwa ni kama shamba la bibi kutokana na kila mtu kuamua kuitumia kwa shughuli zake binafsi ikiwamo ukataji magogo, utengen...