KESI ya mauaji ya watafiti wa Kituo cha Utafiti cha Selian Arusha (SARI) inayowakabili wakazi 29 wa kijiji cha Iringa Mvumi Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, inatarajiwa kutajwa tena Desemba 29, mwaka huu kutokana na upelelezi wake kutokamilika. Watu hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ya mauaji ya watafiti watatu, Nicas Magazine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru huku gari lao lenye namba za usajili STJ 9570 aina ya Toyota Hilux Double Cabin likichomwa moto. Washitakiwa katika kesi hiyo ni Amos Kwanga, Mashaka Nyambi, Victoria Lungwa, Wilson Mabwai, Sarah Chimanga na Daud Mangwata. Wengine ni Peter Fwezi, Adrian Sudai, Charles Lemanya Fredrick Sudai na Tibu Ng’ambi, Bruno Lebedu, Jonas Makwawa,Erasto Masaka, Juma Chitongo, Cesilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa na Juma Madeha. Wengine ni Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga, Yoram Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba. Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa S...
Comments
Post a Comment