Posts

Showing posts with the label SIASA KIMATAIFA

Marekani yaendeleza ubabe Syria, yaitungua ndege nyingine

Image
Marekani imeendeleza ubabe wake wa kuzitungua ndege za kijeshi za Syria mara baada ya kuitungua ndege nyingine isiyo na Rubani kusini mwa nchi hiyo. Marekani inadai kuwa ndege hiyo iliyotunguliwa ya Jeshi la Syria ilikuwa imebeba silaha nzito na hatari kwa Jeshi la Marekani la ardhini hivyo imechukua hatua hiyo kwaajili ya kujikinga na hatari ya kushambuliwa. Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu. Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha juu wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.

Otto Warmbier aaga dunia

Image
Otto Warmbier, mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa. Familia yake imetoa lawama dhidi ya kifo hicho katika kile walichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya Otto aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini . Akiuelezea utawala wa Korea Kaskazini kama ni wa ukatili mkubwa , Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo. Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cincinnati. Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wamesema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.

Chama cha ANC Waanza Kumpinga Rais Zuma..Wataka Achunguzwe kwa Rushwa..!!!

Image
Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimetaka vyombo vya dola kuchunguza barua pepe zilizoibua kashfa ya rushwa kati ya familia ya Rais Jacob Zuma na familia ya wafanyabiashara wakubwa nchini humo ya Gupta. Kwa mujibu wa ANC wameeleza kuwa tuhuma hizo nzito zinapunguza imani na heshima ya serikali yake, hivyo  kashfa hizo hazipaswi kuvumilika au kupuuzwa. Baadhi ya vigogo wa ANC waliungana na upande wa upinzani hivi karibuni wakitaka Rais Zuma ajiuzulu kutokanana na kuandamwa na kashfa za rushwa. Kura za kumtetea zilitosha kumpa nafasi kiongozi huyo kuendelea kuliongoza taifa hilo, huku akiomba radhi kwa kutumia fedha za serikali kukarabati jumba lake kinyume cha sheria. Hata hivyo, wanasheria wa Zuma wameendelea kupinga vikali kashfa hizo kwa madai kuwa barua pepe zilizovujishwa zilikuwa na mkakati wa kisiasa nyuma yake dhidi ya mteja wao. Tuhuma za rushwa kati ya familia ya Rais Zuma na familia ya mabilionea ya Gupta zilidai kuwa familia hiyo ya kitajir...

Vyama vikongwe vyamtangaza kagame kuwa mgombea Urais Rwanda

Image
Katika hatua iliyowashangaza wengi nchini Rwanda vyama viwili vya siasa vikongwe nchini humo vimemtangaza Rais Paul Kagame kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi wa 8 mwaka huu, kabla hata chama chake cha RPF kumtangaza kuwa mgombea wake. Hadi sasa ni wagombea binafsi 3 waliokwishatangaza nia ya kusimama katika uchaguzi huo. Katika mikutano mikuu ya vyama hivyo, chama cha Social Democratic na Liberal Party licha ya kwamba ilifanyika mnamo nyakati tofauti, kauli yao ilikuwa moja, kuunga mkono Rais Paul Kagame wa chama tawala cha RPF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 8 mwaka huu. Hoja iliyotolewa na vyama hivyo pia haitofautiani. Ni kwamba chaguo lao limetokana na pendekezo lililoungwa mkono na wananchi wengi wa Rwanda la kubadili katiba na kumpa rais Paul Kagame uhuru wa kugombea muhula wa tatu kupitia kura ya maoni iliyopitisha katiba mpya mwaka jana. Haya yametokea wakati ambapo hata chama tawala RPF hakijamtangaza Rais Paul Kagame kama mgombea wak...

Trump aiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris

Image
  Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.   Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa. Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira. Amezitaja China na India.  

Akaunti 88 za Rais Jammeh Zafungwa, Waziri wa Serikali Mpya Adai Alikwapua Dola Milioni 50..!!!

Image
WAZIRI wa Sheria wa Gambia, Abubacarr Tambadou, amesema kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Yahya Jammeh, ameiba kiasi cha dola za Marekani milioni 50 kutoka katika kampuni ya mawasiliano ya taifa hilo na tayari mahakama imetoa amri ya kutaifisha mali zake. “Rais Yahya Jammeh yeye binafsi au kwa kutoa maelekezo mahsusi amekwapua dola za Marekani zisizopungua milioni 50,” anasema waziri huyo na kuongeza; “..Jumatatu (Novemba 22, 2017) tumepata amri ya mahakama kuhusu kutaifisha mali zake au kuzizuia.” Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, hii ni mara ya kwanza kwa serikali mpya ya taifa hilo kutoa maelezo rasmi kuhusu wizi alioufanya rais huyo wa zamani aliyeongoza taifa hilo kwa miaka takriban 22 mfululizo. Waziri Tambadou aliwaeleza waandishi wa habari kwamba mahakama ya nchi hiyo imeamuru kufungwa kwa akaunti takriban 88 zenye jina la Jammeh katika benki mbalimbali, sambamba na ‘kuzishikilia’ kampuni 14 zinazohusishwa na mkuu huyo wa nchi wa zamani. Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Ja...

Trump amteua mkosoaji wa Obamacare Tom Price kuwa waziri

Image
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tom Price kuwa waziri wa Afya katika serikali yake. Bw Price, 62,amekuwa katika Bunge la Congress akiwakilisha jimbo la Georgia na ni mtaalam wa upasuaji wa mifupa ambaye amekuwa akiongoza kamati ya bajeti katika Bunge la Wawakilishi. Atatekeleza jukumu muhimu katika mipango ya chama cha Republican wa kubatilisha mpango wa bima ya afya ulioanzishwa na Rais Obama, ambao hufahamika sana kama Obamacare. Wakati wa kampeni Bw Trump aliapa kwamba ataibatilisha sheria hiyo ambayo imekuwa ikitazamwa kama moja ya mambo makuu aliyoyafanya Bw Obama wakati wa utawala wake. Lakini amesema kwamba kuna baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ambavyo atavihifadhi.

Mteule mwengine wa Trump akataa kuchukua wadhfa

Image
Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi. Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake. Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo. Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.

Mugabe Aibuka na Kumtetea Trump kwa Anayofanya,Adai hakutaka Hillary Clintoni Ashinde Uchaguzi..!!!

Image
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba “Marekani iwe ya Wamarekani”. Bw Mugabe, ambaye ndiye mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican . Hata hivyo, amesema hakutaka pia “Madam Clinton ashinde”, akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton. “Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo, Marekani iwe ya Wamarekani – katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,” Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald. Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake. “Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe,” Bw Mugabe amesema.

Huyu Ndiye Trump Bana..Amtumbua Jipu Amshauri Wake wa Karibu Baada ya Kuukosoa Utawala Wake Hadharani..!!!

Image
Mshauri mkuu wa baraza la usalama la taifa la Marekani, amerudishwa kwenye kazi yake ya awali baada ya kukosoa sera za utawala wa Donald Trump zinazohusiana na Latin America. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders, amesema Craig Deare ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Deare alidaiwa kuponda jinsi uongozi wa Trump unavyoshughulika na masuala ya Latin America alipokuwa akizungumza huko Washington. Hii si mara ya kwanza kiongozi wa juu anatumuliwa kwa kumkosoa Trump.