Trump aiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris



 power station chimney (file photo)
Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.
Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump 

Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa.

Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira.

Amezitaja China na India.
  Waandamanaji walikusanyika nje ya ikulu ya White House

Comments

Popular posts from this blog

Kesi Mauaji ya Watafiti Kutajwa Tena Desemba 29

Kimenuka..Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani

INASIKITISHA:Mwanafunzi wa Miaka 13 Abakwa Korongoni Hadi Kufa