Posts

Showing posts with the label BUNGENI

Dodoma: Upinzani Wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Image
Upinzani wamefungua shauri Mahakama Kuu Dodoma wakiiomba mahakama itamke kuwa Spika ataliongoza Bunge kwa kufuata kanuni za kudumu tu. Hii ni baada ya Spika kumzuia John Mnyika kuhudhuria bunge kwa wiki moja ambapo upinzani wamedai hakuna adhabu kama hiyo kwenye kanuni.                              Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.

Bunge latoa pole kwa wanafunzi 32 Waliofariki Arusha

Image
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufuatia vifo vya wananafunzi, walimu na dereva   wa Shule ya Msingi Lucky Vicent, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali leo asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, wilayani Karatu mkoani Arusha. “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa Taifa zima, namuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” amesema Ndugai na kuongeza:   “Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu, vilevile nawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa haraka.”

Zitto Kabwe Aikosoa Serikali Kwa Kuamua Kujenga Reli ya Kati Toka Dar Hadi Moro

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameukosoa mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia Zitto amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa kumtaka Waziri Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa apeleke reli ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine. "Toka mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge wemametoa tafsiri mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni Kigoma Dar es salaam au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni matawi ya reli ya kati...... "Lakini ujenzi wa  'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita za awali unatoka Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri aangalie takwimu ni wapi atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli nyingine....... "Takw...