#BREAKING: Maamuzi ya vyombo vya habari Tanzania kuhusu RC Makonda



Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo March 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo.

TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.

    Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
    Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
    Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.

Unaweza kusoma kila kitu kwenye tamko hili hapa chini.

Comments

Popular posts from this blog

Kesi Mauaji ya Watafiti Kutajwa Tena Desemba 29

Kimenuka..Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani

INASIKITISHA:Mwanafunzi wa Miaka 13 Abakwa Korongoni Hadi Kufa