Posts

Showing posts from February, 2017

Trump amteua mkosoaji wa Obamacare Tom Price kuwa waziri

Image
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tom Price kuwa waziri wa Afya katika serikali yake. Bw Price, 62,amekuwa katika Bunge la Congress akiwakilisha jimbo la Georgia na ni mtaalam wa upasuaji wa mifupa ambaye amekuwa akiongoza kamati ya bajeti katika Bunge la Wawakilishi. Atatekeleza jukumu muhimu katika mipango ya chama cha Republican wa kubatilisha mpango wa bima ya afya ulioanzishwa na Rais Obama, ambao hufahamika sana kama Obamacare. Wakati wa kampeni Bw Trump aliapa kwamba ataibatilisha sheria hiyo ambayo imekuwa ikitazamwa kama moja ya mambo makuu aliyoyafanya Bw Obama wakati wa utawala wake. Lakini amesema kwamba kuna baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ambavyo atavihifadhi.

Mteule mwengine wa Trump akataa kuchukua wadhfa

Image
Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi. Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake. Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo. Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU, Chasema Hakijawahi Dahili Wanafunzi Vilaza

Image
Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) . UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara. “Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza: “Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachuk...

Babu wa Miaka 98 Amuoa Bibi wa Miaka 88 Baada ya Kukaa Miaka 60 Wakichunguzana.

Image
Kweli nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema ukistaajabu ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa Mzee Willy Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60. Hehehe, Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata tamaa, Je ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka hiyo 60, hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy aliupanga huo muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo. Wanandoa hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa wakitembea kwa fimbo. Aidha Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti. “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.” Kwa upande wake Nyambura amesema, amefurahi ku...

Makonda na Sirro Waitwa Mahakamani Leo

Image
                   MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC), Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius Wambura, wamepelekewa barua za mwito za kuwataka wafike Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo. Viongozi hao wamepelekewa mwito huo kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe dhidi yao. Mbowe amefungua kesi hiyo kupinga Makonda kumtaja katika orodha yake ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na dawa za kulevya katika awamu ya pili na kumtaka afike katika Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 10 mwaka huu, kwa ajili ya mahojiano. Katika kesi hiyo Namba Moja ya Mwaka 2017, Mbowe pamoja na mambo mengine, anapinga mamlaka ya RC kumkamata kwa kile anachokiita kudhalilisha watu. Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo na itasikilizwa na jopo la majaji watatu, Sekieti Kihiyo ambaye ni kiongozi wa jopo hilo, akisaidiana na Jaj...

Zitto Kabwe Afunguka...MANJI Sasa Anaonewa na Kudhalilishwa ili Kumkomoa

Image
Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe. Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow? Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahang...

Mugabe Aibuka na Kumtetea Trump kwa Anayofanya,Adai hakutaka Hillary Clintoni Ashinde Uchaguzi..!!!

Image
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba “Marekani iwe ya Wamarekani”. Bw Mugabe, ambaye ndiye mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican . Hata hivyo, amesema hakutaka pia “Madam Clinton ashinde”, akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton. “Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo, Marekani iwe ya Wamarekani – katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,” Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald. Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake. “Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe,” Bw Mugabe amesema.

Huyu Ndiye Trump Bana..Amtumbua Jipu Amshauri Wake wa Karibu Baada ya Kuukosoa Utawala Wake Hadharani..!!!

Image
Mshauri mkuu wa baraza la usalama la taifa la Marekani, amerudishwa kwenye kazi yake ya awali baada ya kukosoa sera za utawala wa Donald Trump zinazohusiana na Latin America. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders, amesema Craig Deare ameondolewa kwenye nafasi hiyo. Deare alidaiwa kuponda jinsi uongozi wa Trump unavyoshughulika na masuala ya Latin America alipokuwa akizungumza huko Washington. Hii si mara ya kwanza kiongozi wa juu anatumuliwa kwa kumkosoa Trump.

Njaa Kali ..Askari Magereza Feki Akamatwa Akiwa na Sare za Polisi Anazozitumia Kuwatishia Watu na Kupanda Nazo Daladala Ili Asilipe Nauli..!!

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata askari feki wa Jeshi la Magereza, Elius Msigwa akiwa amevaa sare za jeshi hilo. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alimtaja kama Elius Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Disemba mwaka jana. Alisema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa na cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti na alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi, kijana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema “Bahati mbaya siku ya juzi sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya kutoka hapa nazirudisha hizi uniform katika...

Pamoja na Kuwa Mgonjwa,Wanachama NCCR -Mageuzi Wamtaka Mbatia Ajiuzulu,Wadai Ni Fisadi Mkubwa Ndani ya Chama Hicho...!!!!!

Image
BADHI ya wanachama wa NCCR-Mageuzi wamemtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na  Katibu Mkuu wa chama hicho, Martin Danda kujiuzulu ndani ya siku tatu kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwamo ubadhirifu wa fedha na kutaka kukiua chama hicho. Mbatia anadaiwa kuuza mali za chama zikiwamo nyumba mbili zilizoko jijini Dar es Salaam eneo la Bunju B, moja iliyoko Tarime mkoani Mara na shamba la ekari 56 lililoko Bagamoyo mkoani Pwani. Faustine Sungura mmoja wa wanachama wa chama hicho, amesema mbali na kuuza nyumba pia Mbatia ana mkakati maalumu wa kuiua NCCR na kuhamia Chadema ambako ameahidiwa ukatibu Mkuu. “Hivi sasa kuna mkakati wa kuuza nyumba nyingine za chama zilizopo mkoani Rukwa na Katavi na mauzo yatakabidhiwa kwake kwa madai kuwa anakidai chama fedha alizokikopesha wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, tunatoa tahadhari kwa watu kutonunua nyumba hizo kwani watapata hasara isiyotibika,” alisema. Pamoja na mambo mengine Sungura amesema viongozi hao wasipojiuzulu atawafunguli...

Kazi Imeanza...Wawili Wapoteza Maisha kwa Kukosa Dawa za Kulevya..!!!!

Image
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea. Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa. "Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wwili wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani" Amesema Sianga Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano kila siku na kwamba hata leo, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa. "Leo asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa kulevya, tupo naye tunaendelea kumuhoji, mengi yataibuk...

News Alert: Mbowe Aitikia Wito Polisi

Image
                                       Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameitikia wito wa Jeshi la Polisi mchana huu, katika kituo cha Polisi kati, Jijini Dar es salaam. tayari kwa mahojiano juu ya tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda

Waziri Mkuu awahimiza wakulima wasiogope kukopa kutoka mabenki

Image
                                  WAZIRI MKUU  Kassim Majaliwa amewataka wakulima wakubwa na wadogo wa miwa kwenye kiwanda cha sukari cha Manyara kuomba mikopo kutoka mabenki kama wanataka kuendeleza kilimo hicho lakini amewasisitiza kuwa ni muhimu kulipa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani katika kijiji cha Matufa wilayani Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara ambapo pia amewaambia zipo nyingi hapa nchini zinazotoa mikopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo. Waziri Mkuu amewataka wakurugenzi wa kiwanda hicho waharakishe uagizwaji wa mitambo mipya ili kiwanda hicho kiweze kuongeza uzalishaji wake uku kufidia pengo lililopo. Aidha amesema takwimu za mahitaji ya sukari hapa nchini zinapaswa kupitiwa kwa sababu hazitoi picha halisi kwani wakati Tanzania ina watu milioni 50 takwimu zinaonyesha...

Kamera Za Uwanja Wa Taifa Kutumika Kuwanasa Watakaong'oa Viti au Kufanya Uhalifu

Image
                      Kwa wale wanaokwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kufanya vurugu hasa wakati wa mechi ya watani, Yanga na Simba itakaypigwa Jumamosi ijayo, waahirishe. Kitengo cha ulinzi uwanjani hapo kimesisitiza kutakuwa na ulinzi mkali pamoja na kamera za ulinzi ambazo ziko tayari kwa kazi. Hashim Abdallah ambaye ni mwamuzi lakini ni askari Polisi, amesisitiza wako imara na kuwaonya weote ambao wanafikiri wanaweza kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kung’oa viti bila ya kujulikana. Kamera za kisasa zitatumika kuwanasa kila watakaofanya vurugu na mara moja hatua za kisheria zitachukuliwa. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyowakutanisha watani hao, mashabiki wa Simba wenye jazba waling'oa na kuvunja kiti hasa baada ya Amissi Tambwe kufunga bao upande wa Yanga. Kabla ya kufunga alishika, lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote na mashabiki hao wakaamua kumaliza hasira zao kwenye viti.

Wasira, Bulaya vuta nikuvute

Image
                       MAJAJI watatu wa Mahakama ya Rufani leo wataanza kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (Chadema) iliyofunguliwa na 'wapambe' wa aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira. Katika kesi hiyo ya mwaka 2016, walalamikaji ni wapigakura wa jimbo hilo ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic Malagila. Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, aliwataja Majaji watakaosikiliza kesi hiyo kuwa ni Salim Mbarouk atakayekuwa Mwenyekiti akisaidiana na Augustine Mwarija na Shaabani Lila. Kwa mujibu wa Msajili Kabwe, walalamikaji hao katika dai lao wanapinga uamuzi ulitolewa na Mahakama Kuu uliohalalisha ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kabwe alisema rufani hiyo itasikilizwa mfululizo na jopo la majaji hao. Pia aliwataja wakili wanaotarajiwa kuwakilishia upande wa walalamikaji kuwa ni C...

Manji sasa anakibiliwa na kesi tatu, nyingine ya Tigo yaibuka

Image
  Manji alinunua kampuni hiyo mwishoni mwa mwaka 2014 na kumalizia malipo mwanzoni mwa mwaka 2015 na kuwa rasmi ya kwake. Tigo iliuzwa kwenye mnada baada ya wamiliki ambao makao makuu yao ni nchini Sweden kushindwa kumlipa mtumishi wao ambaye alikuwa akiisimamia ambaye ni raia wa Uingereza. Baada ya Mwingereza huyo kufungua kesi, waajili hao walishindwa kumlipa, hivyo mahakama ikaagiza kufanyika kwa mnada na kampuni nyingine ya nje ikainunua Tigo kabla ya kumuuzia Manji. Hata hivyo, Manji amekuwa katika misukosuko ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya kutaka mnada urudiwe hali inatakayopelekea yeye kupokonywa kampuni hiyo. “Hii ni kesi ya pili katika zile zinazojulikana ndani ya wiki moja. Lakini wiki iliyopita, kulikuwa na kesi mbili. “Moja ni ya madawa ya kulevya ambayo wanamtuhumu kuitumia, lakini nyingine ni kuhusiana na kutaka kurudiwa kwa mnada wa Kampuni ya Tigo ambayo ameinunua kwa zaidi ya asilimia 90,” kilieleza chanzo hicho cha uhakika. “Kama ulikuwa haujui, Ti...

Sheikh Katimba asema Makonda achunguzwe.

Image
                           JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana na kipato chake halali. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria. Alisema vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa  kufanya uhakiki wa mali za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki. Sheikh Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi anazopewa. Hivi karibuni, Mbunge wa R...

Waziri Mkuu Akuta ya Ajabu Minjingu..!!!

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini. Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Rais  John Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo. Ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilayani Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa. “Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema. “Ni kwa nini mifuko hii in...

Dc Chongolo Ataka Serikali Isipeleke Chakula Cha Njaa

Image
                                    Wananchi wa jamii ya kifugaji hususani vijijini wametakiwa kuacha kulalamika kuna njaa na badala yake watumie mifugo wanayofuga kuuza katika minada na kisha kununua chakula cha kutosha majumbani mwao na kuondoa tafsiri ya kupatiwa chakula na Serikali ili hali wanamifugo. Pia ameitaka Serikali kutowaletea chakula cha njaa,ambapo jamii kubwa imejijengea tabia ya ya kutoacha chakula cha ziada kwa ajili ya Serikali badala yake kutegem,ea kuwa Serikali ittawaletea chakula cha msaada badala yake wabadili mtazamo na tabia zao za kuweza ziada na kuhifadhi chakula endepo kutakuwa na uhaba wa chakula kam hivi sasa kumekuwa na uhaba wa mvua hali ambayo mazao yamekuwa hayastawi kama awali. Hata hivyo katika hoja hizo Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo akatumia nafasi hii kuwataka viongozi wasiwajengee wananchi kuwa kuna njaa na badala yake wawajengee uwezo pindi wanap...

Tundu Lissu asema Serikali haiwezi kuifuta TLS.

Image
Tundu Lissu Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe jana alisema kuwa atakifuta Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society (TLS)) kwa madai kuwa kimesahau misingi yake na kuanza kufanya kazi kama chama cha siasa. Waziri Mwakyembe alisema kuwa, kama wanataka kufanykazi kama chama cha siasa, basi yeye ataongea na msajili wa vyama vya siasa nchini ili cha hicho kipya kisajiliwe. Kufuatia kauli hiyo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na mgombea Urais wa TLS, Tundu Lissu ameandika waraka huu kwenda kwa wanasheria wenzake. Mawakili wenzangu. Mimi binafsi sijashangazwa na kauli ya Dkt. Mwakyembe kwamba ataifuta TLS kama itajiingiza katika harakati za kisiasa. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya Tanzania kutoa vitisho vya kuifuta TLS. Waziri Mkuu hayati Edward Sokoine aliwahi kutishia hivyo katika kilele cha vita dhidi ya wahujumu uchumi miaka ya mwanzo ya ’80. Na hata kabla ya hapo katika miaka ya ’60 na ’70 watangulizi wa Sokoine ...

Manji na Wafanyakazi Wake 25 Kupanda Kizimbani Leo...!!!!

Image
Wafanyakazi 25 wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na  mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, wanaodaiwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini, leo wataanza kujieleza kwa maandishi katika ofisi za uhamiaji. Ofisa uhamiaji wa mkoa, John Msumule  amesema uhamiaji haijawakamata wafanyakazi hao, isipokuwa inashikilia hati zao za kusafiria.  “Kesho (leo) tunatarajia kuanza kuwahoji ili watoe maelezo yao, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani Jumatatu ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua nafasi yake.” Mbali na wafanyakazi hao, Manji anasubiriwa na sekeseke jingine la uhamiaji baada ya kuitwa ili aunganishwe na wafanyakazi hao kushtakiwa kwa madai ya kuajiri wageni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini. Manji amekuwa akishikiliwa na polisi tangu Februari 9 alipoitikia wito wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kuripoti kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Ofisa uhusiano wa T...

Serikali Kupiga Marufuku Pombe za Viroba....

Image
Serikali inatarajia kupiga marufuku utengenezaji na uingizaji wa pombe za bei rahisi maarufu kama “Viroba” Nchini, ndani ya miezi mitatu ijayo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia  kilevi hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya Taifa, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi pamoja na Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2016/17. Dkt. Kigwangalla amesema kuwa baada ya miezi mitatu kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na kuziba mianya yote ya uingizaji wa kilevi hicho ambacho kimekuwa kikitumiwa na vijana wengi, hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa. Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko amesema kwamba pombe hiyo inasababisha vifo vya vijana wengi nchini ambao ndio tegemeo kubwa na nguvu kazi ya Taifa. “Katika kipindi hiki kifupi cha lik...

Mbowe Afunguka ya Moyoni Baada ya Jana Kutajwa na Makonda,Afichua Njama Hizi za CCM kwa Chama Chake..!!!

Image
      Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaita polisi kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, baadhi ya walioitwa wamelaani hatua hiyo wakisema inalenga kuwachafulia majina na heshima mbele ya jamii. Miongoni mwa waliotwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amezungumza na kueleza kutofurahishwa na hatua hiyo. Mbowe aliyekuwa safarini kwenda bungeni Dodoma, alisema ameshangazwa kutuhumiwa kwa jambo asilolijua. “Kama amemtaja mbunge wa Hai anajulikana ni mmoja, hata kama asingesema Freeman, Mbunge wa Hai anajulikana ni Freeman Mbowe. “The only thing (kitu pekee) ninaweza kusema nchi haiendeshwi hivyo. Yametajwa majina mengi ambayo sijui Makonda ana evidence (ushahidi) gani! “Anasema tukiwaita tukiridhika na maelezo yao tutawaachia. Huwezi kusema tu, yaani kwa kusema ni Mbowe... mimi ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mimi ni mbunge, mimi ni mzazi, nina wanachama, maaskofu, mapadri, mashehe na viongozi mbalimbali. “Unapokuwa un...

Kutoka Mahakamni..Ombi la Serikali la Kutaka Lissu Anyimwe Dhamana Latupwa,Lissu Akipewa Dhamana ya Milioni 20

Image
                                  Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi. Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi. Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20