Waziri Mkuu awahimiza wakulima wasiogope kukopa kutoka mabenki

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakulima wakubwa na wadogo wa miwa kwenye kiwanda cha sukari cha Manyara kuomba mikopo kutoka mabenki kama wanataka kuendeleza kilimo hicho lakini amewasisitiza kuwa ni muhimu kulipa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani katika kijiji cha Matufa wilayani Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara ambapo pia amewaambia zipo nyingi hapa nchini zinazotoa mikopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo.
Waziri Mkuu amewataka wakurugenzi wa kiwanda hicho waharakishe uagizwaji wa mitambo mipya ili kiwanda hicho kiweze kuongeza uzalishaji wake uku kufidia pengo lililopo.
Aidha amesema takwimu za mahitaji ya sukari hapa nchini zinapaswa kupitiwa kwa sababu hazitoi picha halisi kwani wakati Tanzania ina watu milioni 50 takwimu zinaonyesha mahitaji ya sukari kuwa ni tani 420,000 kwa mwaka wakati Kenya wako milioni 45 lakini mahitaji yao ni tani 800,000 kwa mwaka.
Comments
Post a Comment