KIBITI Mambo Shwari: Gesti na Viwanja Vyapanda Bei

Maisha ya Kibiti sasa ni shwari hamna shari na tayari bei za vitu kama viwanja na huduma kama za nyumba za kulala wageni (gesti) zimeanza kupanda bei upya kama ilivyokuwa awali. Taarifa hiyo yenye kuashiria dalili njema za kurejea kwa amani na utulivu kwa wakazi wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Pwani, ilithibitishwa na jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa. Hivi karibuni, wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani, zilielekea kuwa tishio jipya la ulinzi na usalama nchini baada ya kuwapo kwa taarifa za mauaji ya kila mara ya watu wasio na hatia, wakiwamo viongozi wa vijiji, vitongoji, polisi na hata raia wa kawaida. Jumla ya watu zaidi ya 30 waliripotiwa kuuawa katika matukio tofauti ya kipindi cha takribani mwaka mmoja tu uliopita. Tishio hilo la usalama Kibiti lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kukimbia na kwenda kuishi maeneo mengine nchini na pia, taarifa zilisambaa hata kwenye mitandao mba...