Posts

Showing posts from June, 2017

TAARIFA ya CHADEMA Kuhusu Lowassa Kuitwa Polisi

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kesho Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano. Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa. Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo. Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa a...

Matamshi ya Magufuli kuhusu wasichana wa shule waliotungwa mimba yawakasirisha wanawake Tanzania

Image
Rais wa Tanzania John Magufuli ameshutumiwa kwa matamshi yake kwamba wasichana wanaojifungua hawafai kuruhusiwa kurudi shule. Ombi la mitandao ya kijamii limewekwa huku shirika moja la wanawake barani Afrika likitoa hamasa ya kumtaka rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo. Bwana Magufuli aliwaonya wasichana wa shule katika mkutano wa hadhara siku ya Jumatatu kwamba ''unaposhika mimba mambo yako yamekwisha''. Sheria iliopitishwa mwaka 2002 inaruhusu kutimuliwa kwa wasichana waliotungwa mimba wakiwa shuleni. Sheria hiyo inasema kuwa wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ''makosa yanayokiuka maadili na ndoa''. Makundi ya haki ya wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali kubadilisha sheria hiyo. Magufuli ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Chalinze ,takriban kilomita 100 magharibi mwa mji wa Dar es Salaam alisema kuwa kina mama hao wachanga hawatasoma vyema iwapo wataruhusiwa kurudi shule. Baada ya kupiga hesabu ,ata...

Mambo 11 Aliyoyapinga Baba wa Taifa Hayati Mwl. JK. Nyerere

Image
                                 Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 13, 1922 katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania karibu kabisa na ziwa Victoria. Alikuwa ni mototo wa chifu Burito Nyerere wa kabila dogo la wazanaki Nyerere alifariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30 asubuhi (kwa saa za Afrika Mashariki), katika hospitali ya Mtakatifu Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa. Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti na busara duniani. Mambo 11 aliyoyapinga baba wa taifa. 1. Ujinga 2. Ubinafsi Na Ufisadi 3. Ubepari 4. Ukabila Na Usehemu 5. Ubinafsishaji Holela Wa Mali Za Umma 6. Kuongozwa Kwa Rimoti Na Nchi Matajiri 7. Uba...

Marekani yaendeleza ubabe Syria, yaitungua ndege nyingine

Image
Marekani imeendeleza ubabe wake wa kuzitungua ndege za kijeshi za Syria mara baada ya kuitungua ndege nyingine isiyo na Rubani kusini mwa nchi hiyo. Marekani inadai kuwa ndege hiyo iliyotunguliwa ya Jeshi la Syria ilikuwa imebeba silaha nzito na hatari kwa Jeshi la Marekani la ardhini hivyo imechukua hatua hiyo kwaajili ya kujikinga na hatari ya kushambuliwa. Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu. Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha juu wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.

Dodoma: Upinzani Wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Image
Upinzani wamefungua shauri Mahakama Kuu Dodoma wakiiomba mahakama itamke kuwa Spika ataliongoza Bunge kwa kufuata kanuni za kudumu tu. Hii ni baada ya Spika kumzuia John Mnyika kuhudhuria bunge kwa wiki moja ambapo upinzani wamedai hakuna adhabu kama hiyo kwenye kanuni.                              Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.

Otto Warmbier aaga dunia

Image
Otto Warmbier, mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa. Familia yake imetoa lawama dhidi ya kifo hicho katika kile walichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya Otto aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini . Akiuelezea utawala wa Korea Kaskazini kama ni wa ukatili mkubwa , Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo. Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cincinnati. Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wamesema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.

CHADEMA Watoa Ushauri kwa Rais Magufuli Sakata la Madini......Wasema Wapo Tayari Kushirikiana Nae

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa kipo tayari kumuongoza Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo madini, huku kikiwataka wananchi kuishauri serikali kuchukua hatua kwanza badala ya kuipongeza kuhusu sakata la Makinikia. Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Chadema, Dkt. Vincent Mashinji amedai kuwa, hatua anazochukua Rais Magufuli kuhusu Makinikia ziko kinyume na Ilani ya CCM ambapo katika ukurasa wake wa 26-28 haikuzungumzia kurekebisha sheria na mikataba ya madini, na kwamba ilani ya Chadema kwenye ukurasa wake wa 57-59 inaonyesha namna ya kuiongoza vizuri sekta ya madini. “Rais hatafaulu vita hii kama serikali yake itaendelea kutubagua au kutosikiliza sauti ya upande wa pili. Pia watu wasiwe wa kutoa pongezi kabla kazi haijaisha. Kama tunatakiwa kulipwa trilioni mia, wajue kwamba za kwetu ni asilimia 4 tu, na hii ndiyo matokeo ya mikataba tuliyoilaani kila siku. mrabaha wetu ni asilimia 4 huku wa...

JPM Avionya Vyombo vya Habari Vinavyowataja Kikwete, Mkapa Sakata la Makinikia

Image
Rais John Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wakiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.  Rais Magufuli ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu baada ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya nchini Canada, Profesa John Thornton. Barrick Gold Corporation ni kampuni mama ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia. “Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike,” amesema  Rais. Ameonya viongozi hao kuhusishwa katika taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia).

Live Updates:Haya Hapa Ndio Mambo Yaliyogunduliwa na Kamati ya Wanasheria na Wachumi ya Kuchunguza mchanga wa Madini

Image
1.Kamati ya wanasheria na wachumi ya kuchunguza mchanga wa madini iliteuliwa Aprili 10 ikiongozwa na Prof. Nehemiah Osoro. 2.Miongoni mwa hadidu za rejea ambazo kamati ilipewa ni kujua idadi ya makotena yaliyosafirishwa nje ya nchi tangu 1998. 3.Kamati pia ilitakiwa kuchunguza kama Tanzania inauwezo wa kutengeneza 'smelter' nchini, gharama zake na muda utakaotumika. 4.Kamati ilitakiwa kuchunguza tofauti ya mapato ambayo Tanzania ilipata na ambayo ilitakiwa kuyapata tangu mwaka 1998. 5.ACACIA inayojinasibu kama mmiliki wa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi haijawahi kuwasilisha nyaraka za umiliki huo. 6. Kamati imebani kwa mujibu wa nyaraka kuwa kampuni ya ACACIA PLC haikusajiliwa nchini 7.Kamati imebaini kuwa wamiliki wa makampuni ya madini nchini wametenda makosa mbalimbali ya jinai. 8.Kamati imeridhia baadhi ya watumishi wa serikali, makampuni ya usafirishaji na TMAA wameliingiza Taifa hasara kwa makusud. 9.Makampuni ya Pangea na Bulyahulu yamepatikana na hatia ya kuliingizia Ta...

Sumaye Nchi Inaendeshwa Kishabiki

Image
                                      WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Sumaye, amesema nchi inashindwa kuendelea kwa sababu inaendeshwa kishabiki  na kwamba mambo yanayofanyika hayana masirahi kwa taifa. FREDRICK SUMAYE. Akizungumza kwenye  Kongamano la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na Umoja wa Vijana wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema (Chaso) jijini Mbeya alipokuwa mgeni rasmi, Sumaye alisema mambo mengi yenye masirahi ya taifa yakifanywa kimzaha yatasababisha madhara kwa taifa. Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, alisema miongoni mwa mambo ambayo ni ya maslahi ya taifa lakini  yanendeshwa kishabiki ni mikataba ya madini na bajeti isiyokuwa na uhalisia. Mengine aliyoyataja ni uendeshaji wa Bunge ambalo kikatiba ni chombo huru ambacho hakipaswi kuiingiliwa n...

Maalim Seif Alaani Adhabu ya Mdee, Bulaya..!!!

Image
                                 Siku chache baada ya Bunge kuwazuia wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya kuingia vikao vyote vya Bunge hadi Bunge la Bajeti mwakani, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema vitendo hivyo ni mwendelezo wa kupigwa mateke kwa demokrasia Tanzania. Pia amesema hiyo ni ishara kuwa watawala waliopewa madaraka hawataki kufuata misingi ya demokrasia iliyopo. Mdee na Bulaya wote kutoka Chadema walikumbana na adhabu hiyo kutokana na vitendo vyao wakati Spika Job Ndugai alipoagiza Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ambaye alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge hili linaloendelea, aondolewe ukumbini wakati wa mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini. Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe, alionekana akimvuta shati mmoja wa askari waliokuwa wakimtoa Mnyika, wakati Bulaya wa Bunda Mjini alionekana akiwashawishi wabunge wa upinzani kutoka nje kuonyesha mshikamano kupinga ua...

INASIKITISHA:Mwanafunzi wa Miaka 13 Abakwa Korongoni Hadi Kufa

Image
Mwanafunzi  wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13 anayesoma Shule ya Msingi Kipanga wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, amebakwa hadi kufa na watu wasiojulikana, ambao waliutupa mwili wake korongoni. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benedict Mapujila alisema kitendo hicho cha kikatili ni cha juzi ya saa 11:30 kijijini humo . Alisema siku ya tukio hilo, mwanafunzi huyo wa kike aliondoka nyumbani kwao kama kawaida yake kwenda shule. Hata hivyo, hakurudi tena kwao na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wazazi wake, kwa kuwa hakuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani. Wazazi wake walikuwa na wasiwasi mkubwa kwa binti yao kuchelewa kurudi nyumbani, hivyo waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji chao. Viongozi hao wa kijiji na wananchi, walianza kumsaka binti huyo kwenye maeneo mbalimbali bila kukata tamaa. “Ilipofika saa kumi na moja na nusu ya jioni waliukuta mwili wa mwanafunzi huyo ukiwa umetupwa korongoni na kubaini kuwa alikuwa amebakwa huku sehemu zake za siri ziki...

Zitto: Tumemtoa Mghwira Ili Kuondoa Dhana Kwamba ACT ni "CCM B"..!!!!!

Image
  Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mghirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B. "Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe. Pia akaongeza kwa kusema kwamba kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.

Ukweli Mchungu..Rufaa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Dhidi ya Adhabu ya Mdee na Bulaya ni Hopeless na ni Kupoteza Muda Tu..!!!

Image
Kuna taarifa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wamekata rufaa kupinga adhabu waliyopewa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya (CHADEMA). Wabunge hao wamefungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha miezi kumi. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Toleo la 2013, Wabunge hao watapokea nusu mshahara na nusu posho kwa kipindi chote cha adhabu yao. Rufaa hiyo, kama ipo kweli, ni hopeless, kupoteza muda na haitafanikiwa. Kuna sababu mbili za kisheria na kiuhalisia. Kwanza, Kanuni za Bunge hazina neno 'rufaa' au 'rufani'. Yaani, hakuna suala la rufaa kwa jambo lolote linaloamuliwa na Bunge (niko tayari kurekebishwa). Katika adhabu zinazotolewa na Bunge, kwa mujibu wa Kanuni ya 74 ya Kanuni za Bunge, hakuna rufaa inayozungumziwa. Kukosekana kwa kifungu maalum katika Kanuni za Bunge kinachohusu rufaa dhidi ya adhabu kwa Wabunge ni pengo kubwa kisheria katika kuwasilishwa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa hiyo inayosemwa kuwasilishwa. Bunge, au Mamlaka iliyopelekewa rufaa, hal...

Hatma ya Mhe Anna Mghwira Kuendelea na Uenyekiti wa ACT Wazalendo Kujulikana Leo..ACT Wakutana Kumjadili..!!!

Image
                                                 Wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekula kiapo Ikulu jijini hapa jana, Jumanne Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitajadili utekelezaji wa majukumu yake mapya na ya uenyekiti wa chama hicho. ACT imesema ilipokea taarifa ya uteuzi huo wakati Mghwira akiwa nje ya nchi hivyo baada ya kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na yeye walifanya mazungumzo kuhusu uteuzi huo. Mghwira aliteuliwa nafasi hiyo Juni 3, mwaka huu na Rais John Magufuli kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadick aliyeamua kuachia ngazi ili vijana waendelee kufanya kazi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Jumanne na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT, Ado Shaibu ni kuwa kufuatia uteuzi huo na uenyekiti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa kamati ya uongozi wa chama...

Lowassa, Sumaye, Mabata Watema Cheche Msibani

Image
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki ya kisiasa.  Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia. “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure." Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “Hata njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu  ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.”  Wakati akitoa salam...

Chama cha ANC Waanza Kumpinga Rais Zuma..Wataka Achunguzwe kwa Rushwa..!!!

Image
Chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimetaka vyombo vya dola kuchunguza barua pepe zilizoibua kashfa ya rushwa kati ya familia ya Rais Jacob Zuma na familia ya wafanyabiashara wakubwa nchini humo ya Gupta. Kwa mujibu wa ANC wameeleza kuwa tuhuma hizo nzito zinapunguza imani na heshima ya serikali yake, hivyo  kashfa hizo hazipaswi kuvumilika au kupuuzwa. Baadhi ya vigogo wa ANC waliungana na upande wa upinzani hivi karibuni wakitaka Rais Zuma ajiuzulu kutokanana na kuandamwa na kashfa za rushwa. Kura za kumtetea zilitosha kumpa nafasi kiongozi huyo kuendelea kuliongoza taifa hilo, huku akiomba radhi kwa kutumia fedha za serikali kukarabati jumba lake kinyume cha sheria. Hata hivyo, wanasheria wa Zuma wameendelea kupinga vikali kashfa hizo kwa madai kuwa barua pepe zilizovujishwa zilikuwa na mkakati wa kisiasa nyuma yake dhidi ya mteja wao. Tuhuma za rushwa kati ya familia ya Rais Zuma na familia ya mabilionea ya Gupta zilidai kuwa familia hiyo ya kitajir...

Vyama vikongwe vyamtangaza kagame kuwa mgombea Urais Rwanda

Image
Katika hatua iliyowashangaza wengi nchini Rwanda vyama viwili vya siasa vikongwe nchini humo vimemtangaza Rais Paul Kagame kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi wa 8 mwaka huu, kabla hata chama chake cha RPF kumtangaza kuwa mgombea wake. Hadi sasa ni wagombea binafsi 3 waliokwishatangaza nia ya kusimama katika uchaguzi huo. Katika mikutano mikuu ya vyama hivyo, chama cha Social Democratic na Liberal Party licha ya kwamba ilifanyika mnamo nyakati tofauti, kauli yao ilikuwa moja, kuunga mkono Rais Paul Kagame wa chama tawala cha RPF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 8 mwaka huu. Hoja iliyotolewa na vyama hivyo pia haitofautiani. Ni kwamba chaguo lao limetokana na pendekezo lililoungwa mkono na wananchi wengi wa Rwanda la kubadili katiba na kumpa rais Paul Kagame uhuru wa kugombea muhula wa tatu kupitia kura ya maoni iliyopitisha katiba mpya mwaka jana. Haya yametokea wakati ambapo hata chama tawala RPF hakijamtangaza Rais Paul Kagame kama mgombea wak...

Baada ya Kutumbuliwa..Prof Muhongo ..Mbunge wa Upinzani Ajitokeza Kumteta..!!!

Image
                                          Mjadala wa mchanga wa dhahabu (makinikia) umeibuka tena bungeni mbunge akiwatuhumu wenzake, huku akimtetea Profesa Sospeter Muhongo kuwa ametolewa madarakani kama vile mbuzi wa kafara. Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea  amesema Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa wawajibike kwa kuwa ni wahusika wa mikataba mibovu ya madini. Amesema makinikia yana dhahabu lakini yanayofanyika yanaweza kuliingiza Taifa kwenye mgogoro wa kidiplomasia, kisheria na wa kimahakama. Kubenea ametoa shutuma hizo jana (Ijumaa) akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/18. Amesema Rais John Magufuli amwajibishe pia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani. Mbunge huyo amesema hapuuzi nia njema ya Rais Magufuli ya kuwatumik...

Waziri Mkuu Awatuliza Wabunge Sakata la Madini ya Mchanga ( Makinikia)

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa madini nchini kuondoa hofu ya kukosa haki zao kwani kamati ya pili iliyoagizwa kufanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi yake.  Waziri Mkuu alisema hayo jana wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka, lililohoji kuhusu taswira ya Tanzania kimataifa hasa katika uwekezaji wa madini. Majaliwa aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa  kamati ya pili iliyoundwa kuangalia athari za kisheria, kisiasa na kimataifa kuhusu sakata la mchanga wa madini bado haijatoa ripoti yake. “Watanzania wengi walikuwa na hofu, hata wabunge wengi katika serikali hii ya awamu ya tano mmekuwa mkizungumzia sakata la mchanga wa madini, lakini niwatoe hofu,  Rais John Magufuli alifanya hayo kwa nia njema ya kulinda rasilimali za Taifa,” amliema Waziri Mkuu aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa  serikali itazingatia ushauri kutoka sekta nyingine kabla ya kuc...

Rais Magufuli awaonya wakwepa kodi

Image
  Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuanzishwa kwa mfumo mpya wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya Kielekroniki, (Data Center) itakuwa dawa kwa wale wote wanaokwepa kulipa kodi. Akizindua uanzishwaji wa mfumo huo, jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema ili kuondoa malalamiko ya wale wanaodai kubambikiziwa kodi isiyo sawa na wale wanaokwepa kulipa kodi, ufumbuzi ni kuwepo kwa kituo hicho. Amesisitiza kuwa ni lazima kila mmoja alipe kodi, ili kuweza kupata mapato yatakayoweza kutumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi. Aidha ameyataka makampuni mbalimbali yaliyoko nchini, yakiwemo ya simu, na Wizara zote kuingia katika mfumo huo mpya wa serikali wa ukusanyaji kodi kwa njia ya kielekroniki, ambao ni muhimu wa ustawi na maendeleo ya nchi.   Rais Magufuli pia amesema kuanzisha kwa mfumo huo ni ukombozi wa kupunguza kero za muungano. ''...Kwa sababu ukijaza vocha yako huko Zanzibar hiyo pesa itaenza Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi hiyo...

Trump aiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris

Image
  Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.   Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa. Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira. Amezitaja China na India.