Polisi Waua Wawili kwa Tuhuma za Ujambazi

 
Polisi wilayani Rungwe wamewaua watu wawili kwa tuhuma za ujambazi baada ya kuanza kufyatua risasi kwa polisi waliokuwa wakiwafuatilia.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Dhahiri Kidavashari amesema leo kuwa  tukio hilo limetokea  katika Tarafa ya Pakati wilayani humo baada ya polisi kuwafuatilia watu waliokuwa na nia ya kwenda kufanya ujambazi  katika duka la mfanyabiashara wa soda na bia za jumla na M-Pesa katika Kijiji cha Kisiba.

Alisema  majambazi watatu walipakizana kwenye pikipiki moja na baada ya kuwaona polisi walianza kufyatua risasi na hatimaye polisi walijibu na kuwajeruhi wawili kati ya watatu huku mmoja akifanikiwa kutimua mbio baada ya kuitupa bunduki.

Comments

Popular posts from this blog

Ikulu ya JPM Yafafunguka Haya Kuhusu Malalamiko ya Kampuni ya Acacia Juu ya Ripoti ya Mchanga wa Madini..!!!

Tathimini ya uharibifu wa kimbunga Debbie yaanza kufanyika Australia

Mbowe Afunguka ya Moyoni Baada ya Jana Kutajwa na Makonda,Afichua Njama Hizi za CCM kwa Chama Chake..!!!