Posts

KIBITI Mambo Shwari: Gesti na Viwanja Vyapanda Bei

Image
                Maisha ya Kibiti sasa ni shwari hamna shari na tayari bei za vitu kama viwanja na huduma kama za nyumba za kulala wageni (gesti) zimeanza kupanda bei upya kama ilivyokuwa awali. Taarifa hiyo yenye kuashiria dalili njema za kurejea kwa amani na utulivu kwa wakazi wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Pwani, ilithibitishwa na jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa. Hivi karibuni, wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani, zilielekea kuwa tishio jipya la ulinzi na usalama nchini baada ya kuwapo kwa taarifa za mauaji ya kila mara ya watu wasio na hatia, wakiwamo viongozi wa vijiji, vitongoji, polisi na hata raia wa kawaida. Jumla ya watu zaidi ya 30 waliripotiwa kuuawa katika matukio tofauti ya kipindi cha takribani mwaka mmoja tu uliopita. Tishio hilo la usalama Kibiti lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kukimbia na kwenda kuishi maeneo mengine nchini na pia, taarifa zilisambaa hata kwenye mitandao mba...

WATU 200 Wakamatwa Kwa Tuhuma za Dawa za Kulevya, Unyang’anyi

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar ES salaam limeendelea kufanya misako na operesheni kali ambapo kuanzia 10/7/2017 mpaka tarde 16/7/2017 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 200 kwa makosa mbalimbali ya uhalifu.

Kimenuka..Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani

Image
Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Mshonzini iliyopo Wilayani Mafia Mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho. Katibu wa CCM Wilayani Mafia, Mohammed Dhikiri, amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema ofisi hiyo imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo na samani za ndani. Bw. Mohammed amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama wa chama hicho. Naye Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dan, amesema, vipo viashiria vinavyoonesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo na kwamba, mtu huyo baada kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakanani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zinavyoonesha.

Sheria Mpya za Madini Mfupa mgumu kwa wawekezaji

Image
                     Wakati Serikali ikiendelea kutafuta njia za kudhibiti kikamilifu rasilimali za nchi baada ya kupitisha sheria mpya ya maboresho ya Sheria ya Madini iliyopendekeza mambo kadhaa, wawekezaji katika sekta hiyo wameanza kutishika na kuanza kujiondoa. Baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo, tayari mwekezaji mmoja kutoka Australia, Ian Middlemas kupitia kampuni yake ya Cradle Resources, amekosa dili la dola 55 milioni za Marekani (Sh121 bilioni) kupitia mradi wa uchimbaji wa madini ya niobium Panda Hill, uliopo nchini. Kufuatia hatua hiyo, wataalamu kadhaa wa masuala ya uchumi wamesema ni lazima sheria hizo zitakuwa zimewashtua wawekezaji. Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (Repoa), Dk Abel Kinyondo alisema watakimbia kwa muda mfupi tu. Profesa Haji Semboja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kutaibuka baadhi ya kampuni ambazo zitafanya hivyo ili kutishia Serikali ili ichanganyikiwe na kub...

MAITI yaokotwa Bwawani

Image
Mwili wa mtu ambaye hajafahamika umeokotwa katika bwawa la maji lililopo Mtaa wa Nkende Shuleni katika Halmashauri ya Mji wa Tarime. Hili ni tukio la tatu la watu kuuawa kisha miili yao kutupwa kwenye mabwawa ya maji katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hivi karibuni, mwili wa kijana ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo hilo hilo. Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo na kubainisha kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanafanya mauaji hayo. Chareles Kisege, ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Nkende Shuleni na James Nyangai mwenyekiti wa mtaa wa Kimusi, wamesema matukio hayo yamezusha hofu miongoni mwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo. Wamitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wauaji hao. Licha juhudi za wananchi kutaka kuuopoa mwili huo, zoezi hilo limekuwa zito na gumu kutokana na kukosa zana. Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda wilayani...

TAARIFA ya CHADEMA Kuhusu Lowassa Kuitwa Polisi

Image
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kesho Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano. Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa. Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo. Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa a...

Matamshi ya Magufuli kuhusu wasichana wa shule waliotungwa mimba yawakasirisha wanawake Tanzania

Image
Rais wa Tanzania John Magufuli ameshutumiwa kwa matamshi yake kwamba wasichana wanaojifungua hawafai kuruhusiwa kurudi shule. Ombi la mitandao ya kijamii limewekwa huku shirika moja la wanawake barani Afrika likitoa hamasa ya kumtaka rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo. Bwana Magufuli aliwaonya wasichana wa shule katika mkutano wa hadhara siku ya Jumatatu kwamba ''unaposhika mimba mambo yako yamekwisha''. Sheria iliopitishwa mwaka 2002 inaruhusu kutimuliwa kwa wasichana waliotungwa mimba wakiwa shuleni. Sheria hiyo inasema kuwa wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ''makosa yanayokiuka maadili na ndoa''. Makundi ya haki ya wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali kubadilisha sheria hiyo. Magufuli ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Chalinze ,takriban kilomita 100 magharibi mwa mji wa Dar es Salaam alisema kuwa kina mama hao wachanga hawatasoma vyema iwapo wataruhusiwa kurudi shule. Baada ya kupiga hesabu ,ata...