Posts

Bunge latoa pole kwa wanafunzi 32 Waliofariki Arusha

Image
Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtumia salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufuatia vifo vya wananafunzi, walimu na dereva   wa Shule ya Msingi Lucky Vicent, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali leo asubuhi katika eneo la Rhotia Marera, wilayani Karatu mkoani Arusha. “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili ni pigo kwa Taifa zima, namuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” amesema Ndugai na kuongeza:   “Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu, vilevile nawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa haraka.”

Zitto Kabwe Aikosoa Serikali Kwa Kuamua Kujenga Reli ya Kati Toka Dar Hadi Moro

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameukosoa mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia Zitto amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa kumtaka Waziri Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa apeleke reli ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine. "Toka mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge wemametoa tafsiri mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni Kigoma Dar es salaam au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni matawi ya reli ya kati...... "Lakini ujenzi wa  'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita za awali unatoka Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri aangalie takwimu ni wapi atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli nyingine....... "Takw...

Mtikisiko wa Uchumi: Benki 3 hatarini kufungwa

Image
  Hali ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga Bancorp. Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria. Hali hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake (TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa uchambuzi wa The Citizen Benki hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia 63. Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka. Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Be...

Mbowe Azua Jipya..Adai Bajeti ya Serikali Haitekeleziki..Wajiandaa Kuipinga Bungeni

Image
                                       Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wataipinga bungeni bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwani haina msaada wowote kwa wananchi wa hali ya chini na wanaamini fedha hizo hazitapatikana kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbowe amesisitiza mwaka jana wabunge wa kambi ya upinzani walieleza wazi kuwa bajeti ya mwaka huu isingetekelezeka na ndio kilichotokea kwani mpaka sasa asilimia 34 pekee ya pesa zote za maendeleo ndizo zimetolewa.

Tathimini ya uharibifu wa kimbunga Debbie yaanza kufanyika Australia

Image
Maofisa katika jimbo la Queensland nchini Australia wameanza kufanya tathimin ya madhara makubwa yaliyosababishwa na kimbuka Debbie, huku baadhi ya maeneo yakiwa hayawezi kufikiwa kutokana na barabara kuharibika na kujifunga kabisa. Baadhi raia wameuelezea mji wa Bowen kwamba umeharibika na kuwa kama ukanda wa vita kutokana na kubomoka kwa majengo na mashamba ya ndizi. Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull, amesema kuwa serikali imejiandaa vyema kukabiliana na madhara ya kimbunga hicho kilichoyakumba maeneo hayo. Hata hivyo mamlaka nchini Austarilia zimeonya kuwa eneo la Pwani ya kaskazini mashariki nchini humo lililopo kilomita 1300 linatarajiwa kukumbwa na mafuriko ikiwa ni matokeo ya kimbunga hicho

Huu Ndio Ujumbe wa Mbunge Husein Bashe wa CCM,Ambao Umekuwa Gumzo Mitandaoni

Image
                            Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe (CCM)amechapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno haya. “Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo‘ “Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu ‘Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru‘ –Hussein Bashe ‘Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu. ‘Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu ‘Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la k...

Madaktari Kenya Wawaonya Madaktari wa Tanzania Wanaotaka Kwenda Kenya

Image
  Chama cha Madaktari wa Kenya (KMPDU), kimewataka wenzao wa Tanzania wasikubali kusaini mkataba wowote wa kwenda Kenya kabla mgogoro wao na Serikali haujatatuliwa. Taarifa ya KMPDU  inasema haina tatizo na uwezo ama mafunzo ya madaktari wa Tanzania na protokali ya leseni za madaktari inayotambulika na Baraza na Bodi za nchi za Afrika Mashariki. “Lakini tunapenda kuwataarifu kwamba kwa miaka miwili iliyopita, madaktari wa Kenya wamekuwa wakihangaika na Serikali ya Kenya kuhusu idadi yetu na kukataliwa kwa kile Serikali na Wizara ya Afya ilichosema ni ukomo wa bajeti jambo ambalo lilikuwa likichochea mgomo uliokwisha wiki moja iliyopita. “Tunawashukuru kwa kutuunga mkono wakati wa mgomo wetu uliodumu kwa siku 100. “Tumeona makubaliano ya Serikali ya Kenya na Tanzania wa kuleta madaktari 500 ili kuleta uwiano (ration) kati ya wagonjwa na madaktari kwenye pengo lililopo nchini kwa sasa. “Hadi kufikia Mei 2017, kutakuwa na madaktari wanaokadiriwa kufikia 1,400 ambao ...