Posts

Trump amteua mkosoaji wa Obamacare Tom Price kuwa waziri

Image
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tom Price kuwa waziri wa Afya katika serikali yake. Bw Price, 62,amekuwa katika Bunge la Congress akiwakilisha jimbo la Georgia na ni mtaalam wa upasuaji wa mifupa ambaye amekuwa akiongoza kamati ya bajeti katika Bunge la Wawakilishi. Atatekeleza jukumu muhimu katika mipango ya chama cha Republican wa kubatilisha mpango wa bima ya afya ulioanzishwa na Rais Obama, ambao hufahamika sana kama Obamacare. Wakati wa kampeni Bw Trump aliapa kwamba ataibatilisha sheria hiyo ambayo imekuwa ikitazamwa kama moja ya mambo makuu aliyoyafanya Bw Obama wakati wa utawala wake. Lakini amesema kwamba kuna baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ambavyo atavihifadhi.

Mteule mwengine wa Trump akataa kuchukua wadhfa

Image
Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi. Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake. Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo. Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU, Chasema Hakijawahi Dahili Wanafunzi Vilaza

Image
Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) . UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara. “Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza: “Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachuk...

Babu wa Miaka 98 Amuoa Bibi wa Miaka 88 Baada ya Kukaa Miaka 60 Wakichunguzana.

Image
Kweli nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema ukistaajabu ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa Mzee Willy Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60. Hehehe, Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata tamaa, Je ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka hiyo 60, hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy aliupanga huo muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo. Wanandoa hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa wakitembea kwa fimbo. Aidha Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti. “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.” Kwa upande wake Nyambura amesema, amefurahi ku...

Makonda na Sirro Waitwa Mahakamani Leo

Image
                   MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC), Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius Wambura, wamepelekewa barua za mwito za kuwataka wafike Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo. Viongozi hao wamepelekewa mwito huo kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe dhidi yao. Mbowe amefungua kesi hiyo kupinga Makonda kumtaja katika orodha yake ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na dawa za kulevya katika awamu ya pili na kumtaka afike katika Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 10 mwaka huu, kwa ajili ya mahojiano. Katika kesi hiyo Namba Moja ya Mwaka 2017, Mbowe pamoja na mambo mengine, anapinga mamlaka ya RC kumkamata kwa kile anachokiita kudhalilisha watu. Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo na itasikilizwa na jopo la majaji watatu, Sekieti Kihiyo ambaye ni kiongozi wa jopo hilo, akisaidiana na Jaj...

Zitto Kabwe Afunguka...MANJI Sasa Anaonewa na Kudhalilishwa ili Kumkomoa

Image
Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua wenyewe. Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha. Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow? Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20% kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia hisa kutoka nje ya Tanzania wanahang...

Mugabe Aibuka na Kumtetea Trump kwa Anayofanya,Adai hakutaka Hillary Clintoni Ashinde Uchaguzi..!!!

Image
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba “Marekani iwe ya Wamarekani”. Bw Mugabe, ambaye ndiye mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican . Hata hivyo, amesema hakutaka pia “Madam Clinton ashinde”, akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton. “Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo, Marekani iwe ya Wamarekani – katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,” Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald. Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake. “Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe,” Bw Mugabe amesema.