Posts

Showing posts from May, 2017

Sakata la Mchanga Lahamia Zanzibar..Wawakilishi Waikaba Koo SMZ..!!!

Image
Msimamo wa baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi juu ya kuizuia Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifungo na Uvuvi ya mwaka 2017-2018 hadi pale watakapopata majibu yenye kueleweka juu ya hatua ya rasilimali ya mchanga kuhodhiwa na Serikali badala ya wananchi wenyewe kama ilivyokuwa awali utapata majibu leo wakati waziri wake, Hamad Rashid atakapojibu hoja zao. Hatua ya wajumbe hao imetokana na malalamiko ya wananchi waliokuwa wakimiliki mashamba ambayo sasa yanachimbwa mchanga chini ya uangalizi wa Serikali huku wao wakiambulia patupu. Awali, mashamba hayo yalikuwa yapo chini ya wananachi ambao walikuwa wakiyatumia kuvuna na kuuza mchanga huo kwa wamiliki wa magari na kampuni mbalimbali za ujenzi. Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said alisema  pamoja na rasilimali hiyo kuonekana kupungua kwa kiwango kikubwa, haikusatahili wananchi kupokonywa mashamba yao bila makubaliano maalumu. Mwakilishi wa Kijitoupele, Ali Suleima Ali ‘Shihata’ alisema utaratibu uliowekwa na Se...

Mtoto Akatwa Makalio na Baba ake

Image
Mwanamume mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemfanyia kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za makalio kwa madai ya utoro shuleni. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo Nuhu (14) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25 Mei, 2017. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni. Kamanda Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili anaofanyiwa mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa kuvumilia na jana (Tarehe 28 Mei.2017) aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upe...

Mapya Yaibuka: Maafisa wa TMAA Walihongwa Mabilioni ya Pesa Ili Smelter ya Kuchanjua Mchanga wa Madini Isijengewe Tanzania..!!!

Image
Kuna mambo mapya yanayozidi kujitokeza tangu rais Magufuli awasimamishe maafisa wakuu wa Taasisi ya TMAA inayosimamia MADINI ambayo pia ilimfanya rais Magufuli kumvua Uwaziri Mh.Muhongo kama Waziri wa Madini kwa sababu zilizo wazi. Inavyosemekana ni kuwa mwaka wa 2009 TUME maalumu iliyojulikana kama PRESIDENTIAL MINING REVIEW COMMISSION,iliyoongozwa na JAJI Mark Bomani. Tume hii ilitoa MAPENDEKEZO kuwa SMELTER ijengwe hapa nchini. Lakini cha kushangaza ni kuwa maafisa hao wa TMAA wakawa tayari wamekuwa COMPROMISED na Makampuni husika yaani WAKAHONGWA ili WANAYAMAZISHE matakwa ya Tanzania Kuwa na UWEZO wake na TEKNLOJIA HIYO. Katika mbinu zao za kuzima ripoti na mapendekezo ya tume TMAA, miaka sita iliyopita hivi wakaanza mipango ya KUYAMWAGIA MAJI mapendekezo YOTE ya Tume ya Jaji Mark Bomani ili KUIDHOOFISHA kabisa Na mwishowe KUZIZIMA kabisa NDOTO za Watanzania kuwa na mitambo yao ya SMELTER. Na hivyo KUTUSALITI sawasawa ili tuendelee KUIBIWA VIZURI na hayo Makampuni. Mwaka wa 2011 MA...

Polepole aonywa kauli yake ya Mauaji Kibiti

Image
Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania  katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi. Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam. Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya. Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa. “Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa ...

Mbowe: Tunajiandaa Kukamata Dola Mwaka 2020...!!!

Image
                               Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wamebadili msingi wa uongozi wao ikiwamo kufanya mfumo unaoendana na mwaka wa Serikali ambao unaanzia Julai Mosi hadi Juni 30. Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema imefanya hivyo kutokana na maandalizi yao ya kushika dola mwaka 2020 na kuwa ndiyo maana wameanza kufanya hivyo mapema. Akifungua mkutano wa Baraza Kuu mjini Dodoma jana, Mbowe aliwataka wajumbe na wanachama kukubaliana na mabadiliko hayo kutokana na hali ilivyo kwa sasa baada ya kuona chama kinakwenda vizuri na kinazidi kukua kila kukicha. “Nasisitiza kuwa, lazima chama hiki tukilinde na kukijenga kwa gharama zote, tumepita milima na mabonde lakini ukweli hata ninyi mnajua kuwa tuko mahali salama sasa,” alisisitiza. Awali, Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji alisema chama kinakua kwa kasi ya ajabu ambayo wengi wanashindwa kuijua. Alisema kwamba mpango walionao ni kuhakikish...

Ikulu ya JPM Yafafunguka Haya Kuhusu Malalamiko ya Kampuni ya Acacia Juu ya Ripoti ya Mchanga wa Madini..!!!

Image
Uamuzi wa Serikali kuhusu suala la usafirishaji wa mchanga wa madini, utategemea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza suala hilo. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa ikiwa ni siku moja baada ya kampuni ya Acacia kuitaka Serikali kuunda kamati huru kuchunguza kiasi cha madini kwenye makontena yake 277 yaliyozuiwa bandarini. Wiki iliyopita, Rais Magufuli alikabidhiwa ripoti na kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ambayo ilibaini kuwa makontena hayo yana tani 7.8 za dhahabu. Pia, Acacia wanadai hawakupewa ripoti ya kamati hiyo licha ya kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi. “Sijui chochote kuhusu hao Acacia kuomba iundwe kamati huru, lakini tunasubiri ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza sakata hili wampelekee ripoti Rais,” alisema Msigwa. Wakati Ikulu ikisema hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alizungumzia ripoti ya kamati ya Profesa Mruma na kusema chanzo cha hayo ni sh...

Hivi Ndivyo Madini Aliyoshtukia JPM Yanavyosakwa Duniani...!!!

Image
WAKATI Rais John Magufuli akikazia msimamo wa kuzuia usafirishaji nje ya nchi makontena ya mchanga wa dhahabu (makinikia), imebainika kuwa baadhi ya madini yaliyotajwa kuwamo katika mchanga huo, yanasakwa kwa udi na uvumba kutokana na umuhimu wake kiuchumi. Aidha, imebainika kuwa mataifa yaliyopiga hatua kubwa kiuchumi kwa kuzalisha bidhaa za kielektroniki kama China na Japan, hutegemea madini hayo katika uzalishaji wa bidhaa kama simu za mkononi, kompyuta, DVD, vifaa vya ndege, betri za magari, satelaiti na hadi utengenezaji wa vinu vya nyuklia. Jumatano iliyopita, Rais Magufuli alipokea ripoti kutoka kwa kamati teule aliyoiunda kuchunguza kila kilichomo katika makontena 277 yaliyoshikiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam ili mwishowe kulinda mapato ya nchi. Matokeo ya ripoti hiyo, iliyowasilishwa na mwenyekiti wake, Prof. Abdulkarim Mruma, yalionyesha kuwa kwa ujumla, thamani ya madini yote yaliyokutwa ni Sh. bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na Sh. trilioni 1.44 kwa kutu...

BAADA ya Kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki..Museveni Ajipa Ziara za Ulaya..!!

Image
                            Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA) baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU), bado halijapatiwa ufumbuzi mpaka hivi sasa. Baada ya Tanzania na Uganda kugoma kusaini mkataba huo wa ushirikiano ambao baadhi ya viongozi wanaufananisha na ukoloni mambo leo, viongozi hao wamekubaliana kutuma ujumbe mjini Brussels, Ubelgiji yaliko makao makuu ya EU ili kujadili kwa kina juu ya EPA na kufikia ufumbuzi. Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni atakwenda huko ili kujadili nafasi ya kiuchumi ya EAC na pia kuzungumzia suala la kutoiadhibu Kenya kutokana na nchi wanachama kutosaini mkataba huo. Akizungumza katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za EAC mara baada ya kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza jumuiya hiyo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Museveni alisema...

UKWELI Mchungu..Ulipumba Unadumaza Demokrasia Nchini...!!!!

Image
                                  KATIKA siasa za Tanzania kuna kupakaziana kwa kila aina, walio madarakani huwakazia wa upande ule wanaoitwa wapinzani. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliitwa chama cha Wachaga kwa sababu mwaasisi wake ni Eddwin Mtei. Hawakusema lolote kwa aliyekuwa Makamu wake, Bob Makani (marehemu) ambaye ni Msukuma wa Shinyanga. Baadaye siku zilivyokuwa zinasogea na Chadema kushika moto Kanda ya Kaskazini, wa upande wa pili wakasema chama cha ukanda kupitia Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti Freeman Mbowe. Ujio wa waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, ukatafsiriwa, wakipewa nchi ni hatari na kwamba wataigawa nchi kikanda. Nadhani ni kutokana na mtazamo huo, Freeman Mbowe akamteua Dk. Mashinji Msukuma kutoka Kanda ya Ziwa, ili kuifuta ile dhana ya Chadema kuwa chama cha Ukanda wa Kaskazini. Kwa upande wa Chama cha Wananchi (CUF), wa upande...

Askofu Gwajima awajia juu wanaoizungumzia nchi vibaya

Image
                             Dar es Salaam.Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaonya baadhi ya watu wanaoiongelea vibaya nchi akiwataka waache mara moja kwa kuwa wanachochea uvunjifu wa amani. Askofu Gwajima amesema kinachotakiwa watu waizungumzie nchi vizuri kwa kuwa amani itakuwepo na uchumi wa nchi utaendelea kukua. "Namkemea yule mtu ambaye anaiongelea vibaya nchi yetu huwezi ukawa unatoa kinywa kinachoashiria uvunjifu wa amani," "Huwezi kila siku unalaani kwa kuiongelea vibaya nchi yetu lazima nikemee ili nchi yetu iweze kuendelea kuwa na amani,"amesema Gwajima katika mahibiri kanisani kwake leo.

Wakandarasi waanikeni wanao waomba Rushwa

Image
                                 SERIKALI imewataka wakandarasi nchini kuwafichua maofisa wa serikali ambao wamekuwa wakiwaomba rushwa ili wawapatie zabuni za ujenzi wa miradi. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Joseph Nyamhanga, wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Mashauriano kwa Wakandarasi mjini Dodoma. Mkutano huo uliofunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, uliandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), na ni wa kila mwaka ambapo wakandarasi hukutana na kuzungumzia changamoto zinazowahusu na kuziwasilisha serikalini. Nyamhanga alisema kuna umuhimu mkubwa wa kushirikiana kupambana na rushwa kwenye utoaji wa zabuni kwani imekuwa ikisababisha miradi kuchelewa ama kutekelezwa kwa kiwango cha chini. “Kwenye hili naomba muipe ushirikiano mkubwa CRB na serikali tuwabaini hawa watu maana wanakwamisha ustawi wa miundombinu yetu, wata...

Update: Wanafunzi Waliofariki Katika Ajali Leo Wafika 32

Image
    Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera. Mkumbo amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo Luck Vicent ya mjini Arusha. Kati ya wale waliofariki 28 walikuwa wanafunzi huku watatu wakiwa ni dereva na walimu wao Ripoti zinasema kuwa basi hilo liliteleza na kukosa mwelekeo ,likatoka katika barabara na kuanguka katika mto katika eneo la Marera eneo la Rhotia, kilomita chache kabla ya karatu katika barabara ya Arusha