Posts

Showing posts from June, 2016

Mtuhumiwa kesi ya Mwangosi akana Ungamo Lake Mahakamani

Image
Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoani hapa, Daudi Mwangosi, Pacificus Simoni ametoa ushahidi wake mbele ya mahakama na kuieleza kuwa alilazimishwa kusaini ungamo mbele ya mlinzi wa amani bila kujua nini kilichoandikwa. Alidai kuwa baada ya kutoka kuhojiwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Ofisa wa Makosa ya Jinai ya Mkoa (RCO), akifananishwa na picha ya gazeti la Mwananchi la Septemba 3, 2012 alipokana siyo yeye, alipelekwa kwenda kufanya ungamo kwa mlinzi wa amani, Frola Mhelela ambaye alikuwa shahidi namba tatu. Alidai wakati anakwenda kwa mlinzi wa amani alisindikizwa na Staff Sajent Erick, ambaye alikuwa ameshika bahasha na kumkabidhi kwa mlinzi huyo. Mtuhumiwa huyo alidai mlinzi huyo alitoa karatasi na kuisoma kisha baadaye alimuambia aisaini, naye bila kuhoji alisaini ile karatasi kwa sababu ilitoka kwa kiongozi wake ambaye ni RCO, Nyegesa Wankyo. Katika kesi hiyo wakili wa utetezi, Rwezaura Kaijage aliiomba Mahakama kwamba mawakili wa upa...

Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli Kuhusu Kauli yake ya Kuvitaka vyama vya Siasa Kuacha Kufanya Kampeni

Image
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kujibu kauli ambayo ametoa Rais Magufuli kuvitaka vyama vya siasa kuacha kufanya siasa mpaka kipindi cha kampeni tena katika uchaguzi wa mwaka 2020. Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kujibu kauli hiyo kwa kuonyesha kusikitishwa huku na kusema kauli hiyo wao kama wazalendo wanaichukulia kama ni vita dhidi ya demokrasia. "Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Tunaichukulia kauli ya Rais Kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya nchi na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu".  Aliandika Zitto Kabwe Mbali na hilo Mbunge huyo aliwataka wanasiasa pamoja na vyama vya siasa kuungana pamoja sasa katika vita hii dhidi ya demokrasia na kuacha tofauti zao ili kuweza kufikia lengo hil...

Ugonjwa Uliozuia Mahafali ya Chadema Wajulikana

Image
Serikali imesema uchunguzi wa awali wa vifo vya watu wanane mkoani Dodoma umeonyesha kuwa vilitokana na familia kula ugali wa unga wa mahindi wenye sumu kuvu B (aflatoxins B). Jeshi la Polisi lilizuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Dodoma ambao ni wafuasi wa Chadema yaliyokuwa yafanyike kwenye hoteli ya African Dream, likisema mikusanyiko yote imezuiwa baada ya kuzuka ugonjwa usiojulikana ambao awali uliua watu sita. Wakati Jeshi la Polisi likizuia mahafali hayo ya Chadema, taasisi nyingine zilikuwa zikiendelea na mikutano kwenye hoteli hiyo, jambo lililowafanya viongozi wa Chadema kulalamikia hafla yao kusambaratishwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na gari la maji ya washawasha. Mbali na kuongezeka kwa idadi ya waliofariki dunia, watu waliougua ugonjwa huo wameongezeka kutoka 21 hadi 28. Naibu Waziri wa Afya, Dk Khamis Kigwangalla alisema pamoja na matokeo hayo ya awali, watalaamu wengine wa afya walienda wilaya za Chemba na Kondoa kuchukua sampuli nyingine. Ali...

GWAJIMA ATOWEKA, POLISI WAZIDI KUMSAKA!

Image
Baada ya kuweka kambi kwa zaidi ya saa saba nyumbani kwa Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Jeshi la Polisi limesema bado linamsaka kiongozi huyo wa kiroho usiku na mchana. Juzi askari wa jeshi hilo, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa zaidi ya muda huo bila kufunguliwa na kuondoka bila kumkamata, hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa chombo hicho cha dola kufanya hivyo katika kipindi cha miezi 16. Baada ya kushindwa kumtia nguvuni mapema mwaka jana, Askofu Gwajima alijisalimisha kituoni siku iliyofuata. Lakini jana, Gwajima hakufanya hivyo,  na haijulikani alipo. Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wanaendelea kumtafuta askofu huyo na kuwataka wenye taarifa za mahali aliko, waisaidie polisi. Akieleza sababu za kwenda nyumbani kwake bila ya kumtaarifu askofu huyo, Kamanda Sirro alisema hawalazimiki. “Si lazima apelekewe taarifa, askari walikwenda kwa nia njema ya kuonana naye ndiyo maana hawakutoa taari...

MARAFIKI WA ISAAC, ALIYEHUKUMIWA KWAKUMTUKANA RAIS ACHANGIWA MILIONI 4.5 YA FAIN

Image
Marafiki wa Isaac Habakuk pamoja na wadau ambao hawakupendezwa na hukumu dhidi yake ya kwenda gerezani miaka 3 au kulipa faini ya milioni 7 kwa kudaiwa kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa Facebook kwa kutumia neno bwege wamemkabidhi jumla ya shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya kulipa faini kuepuka kifungo gerezani. Akikabidhi fedha hizo Jijini Arusha mchana wa leo, mwakilishi wa marafiki hao, Ndg Ephata Nanyaro amesema fedha hizo zimekusanywa kutoka kwa marafiki mbalimbali ambao wametafutana kwa njia ya simu na kila mmoja kuchangia kuanzia sh 500 na kuendelea mpaka zikafika kiasi hicho. Fedha hizo ni makusanyo ya michango ya makundi mawili, moja likiratibiwa na Ephata Nanyaro na lingine likiratibiwa na Malisa Godilistern, wote wanachama wa Chadema na ambao hutumia mitandao ya kijamii kueleza mawazo yao kuhusu mambo mbalimbali. Nanyaro amesema wameamua kufanya harambee ya kumchangia kijana mwenzao aepukane na dhahama ya kutotumikia kifungo kwasababu kwa jinsi sheria ya makosa ya mt...

TAMKO LA ACT-WAZALENDO BAADA YA MKUTANO WAO KUZUIWA NA POLISI.

Image
Baada ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa Chama Cha ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12 2016 kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017. Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni. Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo. Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-...